DARASA LA 1
DARASA UK. 1
WANAFUNZI WA KRISTO:
Mafundisho ya Neema na Kweli ya Kristo
Prophet Joachim Francis
1. WOKOVU NI NINI?
7/22/19, 14:26 – Prophet: Tutaangalia kuwa wokovu ni nini na tutaangalia nini maana ya kuwa Mkristo. Changamoto kubwa ni kuwa watu wengi wanahisi wameokoka lakini hawajaokoka na siyo Wakristo ila wanashiriki sana kwenye nyumba za ibada. Lengo la kufundisha hivi ni kuweka msingi wa kwa nini tunaitwa Wakristo na kuelewa wokovu jambo ambalo ni msingi wa Mkristo yoyote. Cha kwanza kabisa tunachotakiwa kujuwa ni nini maana ya kuitwa Mkristo?
Kuwa Mkristo siyo kwenda kushiriki ibada kila Jumapili; kuwa Mkristo siyo kutoa sadaka… “Mkristo ni kuwa wakala au balozi wa Ufalme wa Mungu duniani.” Ni kwamba, “unawakilisha Serikali ya Mbinguni ukiwa duniani.” Hii haina cha Mchungaji...Nabii...Muinjilisti...wala muumini; hapa kila mtu anabeba Ufalme wa Mungu na anawajibu wakutekeleza mamlaka yake hapa duniani kama ilivyo mbinguni.Yesu ndio muanzilishi wa kuitwa au kupewa neno Kristo...Kristo siyo jina. Maana ya neno ‘Kristo’ ni ‘ALIYEPAKWA MAFUTA / ANNOINTED ONE.’
Kristo ni neno lililo kokotolewa kutoka kwenye lugha tatu...ya Kigiriki, ambayo ni ‘KRISTOS’ ... .Kilatini ambayo ni ‘KRISTHEN’....Kiebrania ambayo ni ‘MESSI / MESSIAH;’ ambayo yanamaanisha, mtu aliyepakwa mafuta. Na katika Agano la Kale waliokuwa wakipakwa mafuta walikuwa ni Wafalme...kwa Wayahudi, Mfalme alikuwa anateuliwa na Mungu kwa kupakwa mafuta na Nabii, kwa hiyo, hakukabidhiwa ufalme hadi hayo mafuta yawe juu yake. Kwa Agano Jipya, Yesu akawa Kristo kwa kupakwa mafuta ya Roho Mtakatifu - Matthew 1:16. Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo’ - Luka 4:17-18. [17]Akapewa chuo cha Nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, [18] ‘Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta’ kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa…'
Prophet: Nataka muelewe kitu kimoja: Roho Mtakatifu sio hayo mafuta ninayozungumzia hapa...bali ni daraja la kupewa hayo mafuta. Nikisema mafuta simaanishi mafuta kama mafuta bali ni ‘Nguvu itokayo kwa Roho Mtakatifu.’ Hiyo nguvu ndio inaitwa ‘Kristo.’ Okay… na nguvu ninayoizungumzia ni ‘UWEPO WA MUNGU.’ Au utukufu wa Mungu...kwa hiyo, Yesu alivokuja duniani; alikuja kurejesha mahusiano ya mwanadamu na Mungu yaliopotea. Warumi 3:23 - Kwa sababu wote wamefanya dhambi, ‘na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;’ pasipo utukufu huu wa Mungu au uwepo wake kuwa ndani yetu, hatuwezi kuwa na mahusiano na Mungu. Kuwa mdhambi maana yake ni ‘kupungukiwa na utukufu wa Mungu’ ...kupungukiwa na utukufu au uwepo wa Mungu ndio kunaitwa ‘MAUTI.’
Adamu alipatwa na ‘mauti’ haya baada ya kutenda dhambi na wote waliokuja baada yake walirithi hali hiyo ya mauti ya kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Warumi 5:12 - Kwa hiyo, ‘kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti;’ na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi… Kwahiyo, kuwa makini sana unavyoanza kuomba maombi ya rehema na kusema kuwa wewe ni mdhambi mbele za Mungu kwa sababu tuliompokea Kristo sio wadhambi tena. Yaani hatupungukiwi na utukufu wa Mungu. Mungu alitupa zawadi ya mwanae Yesu na kwa kupitia huyo tuupokee ‘UZIMA WA MILELE.’ Tunaupokea uzima huo kwa kumuamini Yesu tu.
John 3:16 - Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, ‘bali wawe na uzima wa milele.’ Sasa naomba usome kwa makini hapa: Kwa nini unaitwa uzima wa milele? Kwa sababu tunapokea uwepo / utukufu wa Mungu hapa duniani na baada ya kuondoka hapa duniani kwa hiyo, tunapata guarantee ya kuishi maisha baada ya kifo tena maisha ndani ya utukufu. Kwa hiyo, huu uzima wa milele / utukufu wa Mungu au uwepo wa Mungu, tunaupokea na unakaa ndani yetu...sio madhabahuni...sio kwa watumishi...bali ndani yetu sisi kwa sababu miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu..Roho Mtakatifu anakuja kufanya ibada ndani yetu kwa sababu ya uwepo huo wa Mungu ndani yetu.
1 Wakorinto 6:19 - Au hamjui ya kuwa ‘miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,’ mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe… Hii ndio siri ya Mungu aliyoiweka tangu misingi ya ulimwengu; kuwa uwepo wake utakaa ndani yetu na sisi tutakuwa watu wake. Wakolosai 1:25-27 - [25]ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, ‘nilitimize neno la Mungu; [26] ‘siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;’ [27]ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa,’ nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu…’ Kwa hiyo, ukisema wewe ni Mkristo, maana yake kwanz,a ni kuwa umebeba uwepo wa Mungu/utukufu wa Mungu ndani yako. Ukielewa kuwa umebeba utukufu wa Mungu / uwepo wa Mungu ndani yako, hapo ndio utaweza kuitendea kazi mamlaka ya kifalme iliyo ndani yako.
Nilisema ya kuwa sisi ni Mabalozi wa Ufalme wa Mungu duniani: 2 Wakorinto 5:20 –‘Basi tu Mabalozi kwa ajili ya Kristo’, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Tunakuwa na mamlaka ya kifalme ya Mungu pale ‘tunapozaliwa mara ya pili hapa duniani’ kupitia Neno la Kristo / Ufalme wa Mungu. Tusipo badilisha mifumo yetu ya kuishi kwa kuliamini neno la Ufalme wa Mungu, hatuwezi kuona utukufu wa ufalme huo ukidhihirika ndani ya maisha yetu.
Yohana 3:3 - Yesu akajibu, akamwambia, amin, amin, nakuambia, ‘Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.’ Tunazaliwa mara ya pili hapa duniani...kuzaliwa mara ya pili hakutendeki rohoni...nataka muelewe hiki kitendawili kuanzia leo. Maana, kunatafsiri nyingi za maana ya kuzaliwa mara ya pili...Yesu aliweka hili jambo wazi akimuambia Nikodemo kuwa, anayomuambia ni mambo ya hapa hapa duniani Yohana 3:10, 12 [10] - Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u Mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? [12] ‘Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?’
Kuzaliwa mara ya pili ni kubadilisha mifumo ya kuishi kutoka kwenye mifumo ya kidunia na kuingia kwenye mfumo wa ufalme wa Mungu kupitia kujua neno la Mungu la ufalme wake. Waefeso 1:18-19-[18] Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;’ [19] ‘na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;’…elewa haya mambo huwezi kuona utukufu wa Mungu ukidhihirika ndani ya maisha yako. Kuna matendo ya Mungu lakini kuna utukufu wa Mungu, sasa utaona matendo ila utukufu ndio utakuwa shida kuuona kama hujaelewa ufalme wa Mungu ni nini.
+255 767 540 7**: Its very true na huwa nasikia tunaokolewa kwa neema ya Mungu, je, wokovu unapimwa kwa matendo yako?
Prophet: Wokovu haupimwi kwa matendo yetu. Ephesians 2:8-9 [8] ‘Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;’ [9] ‘wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.’ Anaekuambia kuwa lazima ujitahidi kuonyesha kuwa umeokoka anakutoa kwenye neema ya Mungu. Ukielewa kuwa kuna uwepo wa Mungu ndani yako hapo sasa ndio unapata ahadi ya kumpokea roho mtakatifu kama msaidizi katika maisha yako hapa duniani. Usipo ongozwa au kufunuliwa na Roho Mtakatifu kuna mambo bado utakuwa unashindwa kuyapata kwenye ufalme wa Mungu. Yohana 3:5 -Yesu akajibu, ‘Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia Ufalme wa Mungu.’ Kuzaliwa kwa maji na kwa roho ni kuongozwa na Roho Mtakatifu. Wanaoongozwa na Roho Mtakatifu hao ndio wana wa Mungu, yaani warithi wa ahadi za Mungu katika maisha yao...huwezi rithi ahadi za Mungu pasipo ya kuongozwa na Roho Mtakatifu au Roho wa Mungu...na kusudi la kuongozwa na Roho wa Mungu ni ili upate kujuwa yaliyo yako katika Ufalme wa Mungu.
1 Wakorinto 2:12 – ‘Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, kusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.’ Kila kitu unachokihitaji Mungu alishakupa ila sharti ya kuyapokea ni kwa kumsikiliza na kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu kwa sababu yeye pekee ndio anajuwa Mapenzi ya Mungu kuhusiana na maisha yako....sio Nabii...sio Mchungaji au mtumishi yeyote…
‘Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu,
kusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.’
Warumi 8:26-27-[26] Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. [27] ‘Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu sawa sawa na mapenzi ya Mungu.’
1 Wakorinto 2:10-11 - [10] Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. ‘Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.’ [11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? ‘Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.’
Prophet: Kwa hapa nimemaliza kufafanua kuhusu Maana ya Mkristo. Mwenye swali anaweza uliza, +255743238599. Nitaendelea tena kufundisha somo jingine.
+255 713 626 4**: Asante sana barikiwa.
+255 654 333 5**: Barikiwa sana mtumishi. Mimi nauliza, kuna hii notion kuwa "wakiookoka wanahitaji kuishi maisha ya toba kila dakika; kila siku, maana kama binadamu hatujakamilika hivyo inabidi kuokoka kila siku...hii sasa unaizungumziaje?
Prophet: Hii sio sahihi kwa sababu hatuombi Mungu atusamehe kila mara, tunapokea msamaha mara moja. Kama ikitokea tumekosea, biblia haisemi tuombe rehema. Biblia haisemi hivyo. Inasema, tunae muombezi kwa Mungu kwa ajili ya makosa yetu. Matendo 26:18 – ‘uwafumbue macho yao, na kuwageuza waliache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapokee msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
1 Yohana 2:1-2 - (1) Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhamb,i tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, [2] naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
+255 654 333 5**: Kwa sababu ya Yesu.... Na kwa sababu sisi wanadamu tu wadhaifu, Mbingu ipo kwa ajili ya wale watu ambao Mungu anawahesabia haki kwa Neema yake kupitia Yesu Kristo.
1) Wote ambao hawakuamini na hawatamwamini Yesu
2) wote wanaoijua kweli na hawaifuati
3) Wote wanaoigiza wokovu
4) Wote wanaomkufuru Roho Mtakatifu
5) wote wasioishi maisha ya toba ni wa jehanamu.
Maisha ya toba si tuu swala la kuomba msammaha ila kuendelea kujitakasa katika Damu ya Yesu.
+255 654 333 5**: barikiwa sana angalia hayo mafundisho hasa paragraph ya mwisho "si tu swala la kuomba msamaha ila kuendelea kujitakasa kwa damu ya yesu"
+255 767 540 7**: Asante mtumishi.
Prophet: Hii inaonekana nzuri ila sio mafundisho ya kweli. Haipo kwenye NENO kabisa. Labda niseme TOBA ni nini.
Toba sio kuomba msamaha. Toba ni kubadilisha mtazamo, nia, fikra zako na kuzielekeza kwenye NENO la Mungu. Sio kuomba Damu ya Yesu ikutakase kila dakika; kila siku; kila ukitaka kuomba. Damu ya Yesu ilitutakasa mara moja pale alipokufa msalabani. Tunachotakiwa ni kupokea msamaha huo mara moja basi. Hatuhitaji kuomba utakaso kila siku: Utakaso ulishafanyika Calvary, ni swala la kuamini tu kuwa umetakaswa. Waebrania 9:28 - kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Waebrania 10:10 - Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
+255 686 361 1**: Amina!
+255 654 333 5**: Amina!
+255 654 333 58**: Aisee, ni kweli kabisa...
+255 767 540 7**: Hii kwa kweli huwa inanichanganya sana, hivi kwa mfano mtu ametenda dhambi ya kusema uongo, je, hatatakiwa kutubu bali kuamini tu kuwa Yesu alisha msamehe Calvary? Naomba msaada hapo mtumishi.
Prophet: Ndivyo neno linavyosema. Tatizo ni mapokeo tuliyopewa.
+255 767 540 788: Ok, asante mtumishi.
Prophet: Hakuna mahali tumeambiwa tuombe utakaso sababu maombi yetu hayawezi kutukasa. Hapa ndio tunatakiwa kuelewa kuwa tumesamehewa kwa neema. Tukielewa hivyo, hata kutenda dhambi itakua ngumu.
Laura: Ameeeen, Leo nimejifunza kitu kikubwa saaana. Barikiwa mtumishi. Pia nina swali...inakuwaje kila tukiiingia kanisani tunaongozwa sala ya toba jamaaani? Tutachanganyikiwa aiseeee…
Prophet: Ni mapokeo tu hayo.
Laura: Kwa hiyo, tunavyokuwa tunaomba; tunakuwa tunapiga kelele tuuu au Mungu anatuangalia?
Prophet: Ni kwamba, tumefundishwa kuomba maombi yasiokuwa na ufahamu wa NENO la Mungu. Ukisema, eeh Mungu mimi ni mwenye dhambi, nisamehe, nitakase: unamaanisha hujaokoka bado. Na huamini kuwa, Yesu alikufa ili utakaswe.
Laura: Aaaaaaaah!
Prophet: Haifanyi Mungu akuhurumie, sana sana anakuona unaangamia kwa kukosa maarifa.
Laura: Leo ndio leo!
Prophet: Kwa sababu Mungu anaangalia NENO lake alitimize, sio makelele ya maombi yako.
+255 719 513 9**: Somo zuri sana my prophet, nimebarikiwa.
Prophet: Amina!
+255 719 513 9**: Amen!
Laura: Prophet Jo, kusema kweeeli tumekaririshwa saana na masomo haya hawatufundishi kabisaaa!
Prophet: Shetani anajuwa; watu wakijuwa haya, ataacha kuwasumbuwa!
+255 719 513 9**: Umeona hawatuambii ukweli…
Laura: Wametufundisha juu juuu tuuu… hawachambui kama hivi.......wooii; mimi washanichoshaa kabisaa maana kila siku mapya… Kweli kabisaaa mtumishi, wewe tufundishe tuuu na Mungu atakubariki ili tukienda katika makanisa, tujuwe jinsi yakuwakimbia… na mafundisho hewaaa..
+255 686 361 1**: Wanajuwa wakitufundisha tutafunguka kwenye kila Nyanja; ndio maana wanatufundisha kutoaaa tuuu! Wanatutishia na kutoa, Mungu atusaidie, asante sana Prophet.
Prophet: NAMNA YA KUOMBA iliyo sahihi. Nataka nifundishe kwa ufupi kabla hamjapumzika, sababu najuwa mtaomba.
+255 686 361 1**: Sawa!
Prophet: Cha msingi, cha kuangalia kabla ya kuomba, ni kuchunguza nia inayokufanya uombe.
Cha kwanza kabisa, nataka mfahamu ya kuwa, maombi sio kumpa Mungu taarifa. Maombi ni ukiri. Maombi sio kumbembeleza Mungu akufanyie mambo Fulani. Mungu anajuwa mahitaji yako. Kwa hiyo, mambo ya muhimu ya kuchunguza kabla hujaomba ni, je, nia gani imekufanya uombe. Na unaamini unacho kiomba? Maombi yoyote unayofanya yatajibiwa kama ukiwa na nia iliyo sahihi na ukiri unaotokana na imani. Matthew 7:7 - [7] Ask, and it shall be given to you; seek, and ye shall find; knock, and it shall be opened unto you: ‘Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;’
+255 785 918 6**: Amen!
Prophet: Maombi yoyote yana kanuni tatu ambazo ni:
- Omba kwa Imani
- Omba kwa ajili ya mapenzi ya Mungu yatimie
- Omba kupitia jina la Yesu
Kuomba kwa imani kukoje? Kuomba kwa imani ni kuamini kuwa umeshakipokea ulichokiomba: Marko 11:24 - Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Usipo amini kuwa unachokiomba umeshakipokea; hutakipata kwa sababu hujaomba kwa imani.
+255 785 918 6**: Amen!
+255 785 918 6**: Mungu atusaidie!
+255 686 361 1**: Amen!
Prophet: Cha pili, ni kuwa, hakikisha kuwa, unachokiomba, ukikipata, kitamrudishia Mungu utukufu! Yakobo 4:3 - Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. 1 yohana 5:14-15 - [14] Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. [15] Na kama tukijuwa kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
Vesta: E Mungu tusaidie sie tusioelewa maandiko yako, maana, tunalishwa vitu tusivyovielewa kabisa!
Prophet: Usiombe upate mambo ambayo utayatumia kwa ajili ya faida yako tu, hutapokea.
Vesta: Amen!
Prophet: Kuomba mapenzi ya Mungu yatimie, ni kwamba, unaomba ya kuwa, chochote utakachokipata kitumike pia kuendeleza Ufalme wa Mungu.
+255 785 918 6**: Kwa kweli, kumbe!
Vesta: Amen!
Prophet: Ya tatu, ni kuwa, omba kwa jina la Yesu. Yesu alisema kuwa, yeye ndio njia ya kweli na uzima. Hakuna anaeweza kufika kwa Mungu pasipo yeye kwa hiyo, yeye ndio mlango.
Aliposema kuwa, bisheni nanyi mtafunguliwa; alimaanisha kuwa, ombeni kupitia jina Lake Tu.
Yohana 14:6 - Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. John 14:6,13-14 - [6] Jesus saith unto him, I am the way, the truth, and the life: no man cometh unto the Father, but by me. (Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.) Yohana 14:13-14 - [13] ‘Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. [14] Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu. Yohana 16:23-24 - [23] Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, ‘Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.’ [24] ‘Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.’
Prophet: Sasa ukiomba kwa jina la mtumishi unayempenda na kumuamini hapo ndio unapoteza address kabisa! Unaingia kwa miungu mingine. Kwa hiyo, ukiomba, hakikisha unajuwa na kuamini kuwa Mungu ni Baba yako; anakupenda na unamahusiano naye na unajuwa utapata unachokiomba kwa imani...usipojuwa kuwa Mungu ni Baba yako; ni bora usiombe kitu maana hadi hapo hautakuwa unaelewa kuwa unamahusiano na Mungu ambaye ni Baba yako...ndipo hapo unasikia watu wanaomba rehema sababu wanahisi Mungu amewakasirikia!
Mathayo 7:8-11 - [8] ‘kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.’ [9] ‘Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?’ [10] ‘Au akiomba samaki, atampa nyoka?’ [11] ‘Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajuwa kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?’ Ukiomba kwa namna hii, utafurahia maisha yako ya maombi na maombi hayatakuwa mzigo kwako.
+255 719 513 9**: Amina!
+255 713 626 4**: Nimelewa sasa!
+255 713 626 4**: Mimi naona siyo kwamba hawatuambii ukweli na wenyewe pengine hawajui! Asanteeeee mtumishi!
+255 6543335**: Mimi nionavyo, kweli kila mtu ana mapokeo tofauti. Sijui tufanyeje, ifike mahali sasa wakristo wote tupate mapokeo sahihi na sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Maana, utakuta kila makanisa yana mapokeo yake.
Prophet: Na ndio maana maisha wengi ya wakristo hayana matokeo mazuri kwa sababu wanaaminishwa tofauti na mapokeo ya Kikristo.
+255 654 333 5**: Aisee, tunahitaji uweza wa Mungu atusaidie tutoke katika janga hili.
+255 654 333 5**: Nina swali. Mtoto mdogo anapobatizwa, hivi huwa ni batili? Nikiangalia makanisa yetu mengi watoto hubatizwa wakiwa wachanga au wadogo.
Prophet: Okeee, hapo sasa inabidi nizungumzie UBATIZO NI NINI? Kwa sababu, watu wengi wameaminishwa kuwa ubatizo ni ubatizo wa maji ndio maana hata unaona watoto wadogo wanabatizwa. Nitaleta maandiko ila kwa ufupi kabisa.
Wakristo hatubatizwi kwa maji...
Ubatizo wetu ni kwa njia ya imani kwa kumpokea Roho Mtakatifu na kupata nguvu zake ndani yetu. Ili tumpokee Roho Mtakatifu, tunatakiwa tuamini ubatizo wa Yesu Kristo. Hapa sasa ndio kwenye changamoto kubwa...ubatizo wa Yesu ni nini? Ubatizo wa Yesu ni kufa na kufufuka kwake. Usipo amini katika kufa na kufufuka pamoja na Yesu huwezi mpokea Roho Mtakatifu. Haya nilete maandiko kwanza: Luka 3:16 - Yohana alijibu akawaambia wote, ‘Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;’ kwa hiyo, inamaana, Yesu hakuja kuanzisha ubatizo wa Maji, hapana! Alikuja kuanzisha ubatizo wa kiroho. Kwa hiyo, hapa swali linaweza kuja kuwa: kwa nini Yesu alibatizwa kwa maji?
Okee, Yesu alibatizwa kwa maji mengi kama ishara na unabii wa kufa na kufufuka; sio kwamba ili watu waanze kubatizwa kwa maji mengi kama mapokeo. Kwa hiyo, wanaobatiza kwa maji mengi ni wale wanajuwa tu kuhusu ubatizo wa Yohana na sio ubatizo wa Yesu wa Roho Mtakatifu. Matendo 18:24-26 - [24] ‘Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.’ [25] Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, ‘alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijuwa ubatizo wa Yohana tu. [26] Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukuwa kwao, ‘wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.’
Kwa hiyo, huyu mtumishi alikuwa akihubiri habari za Yesu ila alikuwa akijuwa kuhusu ubatizo wa Yohana wa maji tu. Kwa hiyo, ubatizo wa mkristo ni ubatizo unaopatikana kwa njia ya kuamini. Wakolosai 2:12 – ‘Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.’
Vesta: Kwani sisi Waafrika tunakosea wapi?
Prophet: Hapa ndio kuna maana halisi ya ubatizo, ngoja nifafanue vizuri.
Vesta: Kweli tunalishwa matango pori, Mungu tusaidie kujuwa maandiko yako na kuelewa.
Prophet: Usipoamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na tukafa pamoja naye kiroho, akafufuliwa na Roho Mtakatifu na tukafufuka pamoja naye katika ulimwengu wa roho na kuketishwa juu sana pamoja na Mungu, huwezi pokea nguvu za Roho Mtakatifu.
Vesta: Kweli kabisa!
Prophet: Hili nitakalo lisema hapa ndio msingi wa imani Yetu kama wakristo kuwa, Yesu alikufa; tukafa pamoja naye; akafufuka, tukafufuka pamoja naye. Wakolosai 1:23 – ‘mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake. Wakolosai 2:4, 6-8 - [4] Nasema neno hili, ‘mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi. [6] Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; [7] wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. [8] ‘Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.’
Warumi 6:3-5,8 - [3] ‘Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?’ [4] ‘Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.’ [5] Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; [8) ‘Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;’ Kwa hiyo, usipo amini kuwa tuliifia asili ya dhambi na kupokea uzima kupitikia Roho Mtakatifu, ni ngumu sana kuishi maisha ya ushindi kupitia nguvu za Mungu...na hakuna nguvu za Mungu zingine unazoweza kuzipata pasipo kuamini kweli hii. (Kama unataka upako huo, upo hapa.)
1 wakorinto 15:14, 17 - [14] ‘tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.’ [17] ‘Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.’ Kwa hiyo, usipo amini hili na kama hulijui hili na unaenda kanisani bado sio mkristo. Hili sio somo la leo ila tu nimejibu swali lililo ulizwa hapo juu. Ingawa linagusia vipengele vya leo.
+255 785 918 6**: Amina!
+255 654 333 5**: Nashukuru sana Mtumishi wa Bwana...sasa hili somo nimelielewa. Kwa hiyo, kwa wale wanaonatizwa kwa maji mengi ni kama wana enzi ubatizo wa Yohana...inasemekana upo powerful sana kiasi ukizama katika maji, ukiibuka unajazwa Roho Mtakatifu hapo hapo.
Prophet: Hapana utatoka tu umeloa maji!
+255 654 333 5**: Yaani wakikusikia wenye ubatizo wao, hawatakuelewa! Wenyewe wanatoa shuhuda zao baadhi yao siku hiyo waliyobatizwa tu waliibuka na Roho Mtakatifu.
Prophet: Unajua watu wengi wanachanganya hisia na nguvu za Roho Mtakatifu. Ukitaka kujuwa, wafuatilie baada ya siku mbili tatu utaona.
+255 654 333 5**: Jana kuna mtumishi mmoja wa kanisa moja wapo la wanaobatizwa kwa maji mengi...alisema, ubatizo wa kweli ni wa maji mengi…hakuna mwingine zaidi…tena with confidence…
Prophet: Sasa changamoto ni kufahamu maandiko…
+255 654 333 5**: Kweli Mungu atusaidie, maana, Jumamosi kuna mtu nyumbani kwangu anaenda batizwa ubatizo wa maji mengi, akiambiwa huo ndio wa kweli kabisa...
Prophet: Mungu atusaidie kwa kweli! Tunaishia hapa kwa leo. Tutaendelea na sehemu ya pili ya somo letu tukiangalia juu ya AHADI ZA MUNGU.
XXXXXX
Comments
There are no comments yet!